Return to Index

148

149

Haya umati wa Yesu

150
SongInstrumental
	

1. Haya, umati wa Yesu, Ulioungwa naye! Haya, enendeni hima Katika vita kubwa! Shetani tayari, Kupigana na sisi! 2. Tumfuate Yesu Kristo, Tumwamini yeye tu. Mwovu akituvizia Sisi hatuogopi. Majeshi ya mbingu Ni pamoja na sisi! 3. Tukikesha na kuomba Yesu anayotaka, Tukishika neno lake Na kumtegemea Kwa nguvu hizi tu Tutaweza kushinda! 4. Sasa haya wenzi wangu, Tumfuate Yesu tu! Siku za maisha yetu, Tuwe katika yeye. Tuache dunia Kuingia mbinguni! 5. Pale Mungu atawapa Taji walioshinda, Wapate urithi wao Nyumbani mwa milele. Hayani! Tuimbe, Tumsifu Bwana wetu!