Return to Index

149

150

Haya ee moyo wangu

151
SongInstrumental
	

1. Haya ee moyo wangu, imba kwa furaha. Umwimbie Muumbaji mbingu na dunia. Atukuzwaye pote umsifu na wewe kwa nguvu zako zote, umri wako wote. 2. Mungu wake Yakobo. ndiye Mungu wwetu. Ukimchagua yeye, una fungu jema, unacho kitu chema, umepata mali; moyo utakung’aa shida zitakwisha. 3. Ni mwenye nguvu nyingi, hana amshindaye, kwa hekima aumba vyote ni ajabu, misitu na mabonde, milima,mashamba, vilivyo baharini wanyama porini. 4. Ana mizungu mingi, kuponya wanawe. Anawapa riziki, hata siku za njaa. Wenye chakula haba wanenepa miili: hata waliofungwa anawafungua. 5. Mashangilio yote hayamtoshi yeye. Ni mwema peke yake nami ni vumbi tu! Ananihurumia kwa kuwa ni wake, kwa hiyo nalikuza Jina lake pote.