Return to Index

29

30

Nilikuwa kondoo aliyepotea

31
SongInstrumental
	

1. Nilikuwa kondoo aliyepotea, Sikupenda zizi kamwe, ila kutembea Nilikuwa mwana asiyesikia, Sikupenda baba yangu wala kutulia. 2. Na mchunga mwema alinitafuta, Baba kwa mapenzi ndiye aliyenivuta; Karibu ya kufa, kwa kiu na kwa njaa, Waliniona mnyonge, waliniokoa. 3. Yesu ni mchunga, mwenziwe hapana, Aliosha taka zangu, dhambi nyingi sana; Kwa vidonda vyangu alitia dawa. Ndiye aliyenipata, na kwake nalindwa. 4. Nilikuwa kondoo aliyepotea Sasa nampenda Baba, na mchunga pia; Kwanza nilitanga na kukosa sana, Hivi nyumbani mwa Baba sipotei tena.