Return to Index

30

31

Msingi imara enyi wa kweli

32
SongInstrumental
	

1. Msingi imara, enyi wa kweli, Umekwisha pigwa kwa neno hili; Aongeze lipi? Mnayo pia Kwa Yesu mliomkimbilia. 2. Wambiwapo vuka maji ya giza, Mito ya mashaka taipunguza; Takupa nawe, nikuwezeshe, Ipata kufaa, isikutishe! 3. Utakapopishwa ndani ya moto Nnguvu nitakupa, upate pato; Huteketezwi, ila taka zako, Na zitasalia dhahabu zako. 4. Hata zije mvi, walio wangu Hawaoni kwisha mapenzi yangu; Nazo zitakapowenea, ndipo Mabegani mwangu niwatwekapo. 5. Na mtu aliyenitegemea Kamwe kwa adui sitamtia; Nguvu za jehanam zijapotisha, Mtu wangu kamwe sitamuacha.