Return to Index

5

6

Baba Mwana Roho Mungu mwenye

7
SongInstrumental
	

1. Baba, Mwana, Roho, Mungu mwenye enzi, Kila tukiamka tunakuabudu Baba, Mwana, Roho, Mungu wa mapenzi, Ewe Utatu, tunakusifu. 2. Baba, Mwana, Roho, wakuaminio Wanakutolea shukrani zao Wanakusujudia malaika nao: Wewe u mwanzo, nawe u mwisho. 3. Baba, Mwana, Roho, sisi tu gizani, Utukufu wako hauoni kosa; U Mtakatifu, nawe u mapenzi, U peke yako, mwenzio huna. 4. Baba, Mwana, Roho, Mungu mwenye enzi, Ulivyoviumba vyote vyakusifu: Baba, Mwana, Roho, Mungu wa mapenzi Ewe Utatu, tunakusifu.