Return to Index

59

60

Waponyeni watu wamo kifoni

61
SongInstrumental
	

1. Waponyeni watu wamo kifoni, Watoeni walio shimoni; Na aangukaye mumzuie; Ya Bwana Yesu wahubirini. Walio kifoni waokoeni, Mwokozi yuko, wahubirini. 2. Wajapokawia anangojea, Awasubiri waje tobani; Msiwadharau, muwaonyeni; Huwasamehe; wakiamini. 3. Myoyoni mwa ndani, yule shetani Ameyaseta mawazo yao; Lakini kwa Bwana huwa mazima, Tukiwavuta kwa pole hao. 4. Kawaokoeni, wale njiani, Mutimize mapenzi ya Bwana; Na kwa nguvu zake warudi kwake, Kwa subira waonyeni sana.