Return to Index

82

83

Kwa wingi wa nyama

84
SongInstrumental
	

1. Kwa wingi wa nyama, Na sadaka pia, Hupata wapi salama, Kwondoa hatia? 2. Sadaka ni Yesu, Hwondoa makosa; Dhabihu mwenye jina kuu, Atanitakasa. 3. Kwa yangu imani, Nikuweke sasa Mkono mwako kichwani Kukiri makosa. 4. Roho yakumbuka Mambo ya mtini, Mzigo ulijitweka, Ndiyo yangu deni. 5. Deni hutanguka, Tukimuamini; Kwa damu tumeokoka, Twimbe furahani.